‘LIGI KUU NDOGO’ KUPIGWA KAMBARAGE KUANZIA JUMAMOSI

Unknown | 10:51 PM | 0 comments


Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
CHAMA cha Soka Shinyanga (SHIREFA), kwa kushirikiana na kampuni ya Cleverland Res ya Mwanza, wameandaa mashindano maalum ya timu za Ligi Kuu za Kanda ya Ziwa Victoria.
Mratibu wa mashindano hayo, Kabole Kahungwa ameiambia  kwamba michuano hiyo itashirikisha timu zote za Kanda ya Ziwa zilizopo Ligi Kuu na yatafanyika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Amezitaja timu hizo kuwa ni Stand United, Mwadui FC zote za Shinyanga, Toto African ya Mwanza na Kagera Sugar ya Bukoba.
Kikosi cha Stand United kilichoshiriki Ligi Kuu msimu uliopita

Kahungwa, mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba SC ya Dar e Salaam amesema mashindano hayo ni maalum kwa ajili ya kuzipa maandalizi timu za Kanda ya Ziwa kabla ya Ligi Kuu.
“Kama unavyoona timu za Kanda ya Ziwa zimefanya usajili mzuri kuelekea Ligi Kuu, kwa hivyo na sisi tukaona tuziandalie mashindano baina yao ili kujiweka fiti,”amesema Kahungwa.
Ligi Kuu inatarajiwa kuanza wiki ya pili ya Septemba na Kanda ya Ziwa msimu huu itakuwa na nne, kutoka mbili za msimu uliopita Kagera Sugar na Stand United, baada ya kupanda kwa Toto na Mwadui.

AGOSTI 8, 2015
Stand United Vs Mwadui FC
AGOSTI 9, 2015
Toto African Vs Kagera Sugar
AGOSTI 10, 2015
Mwadui FC Vs Toto Africans
AGOSTI 11, 2015
Kagera Sugar Vs Stand United
AGOSTI 12, 2015
Stand United Vs Toto African
AGOSTI 13, 2015
Mwadui FC Vs Kagera Sugar
 
 
Chanzo: Bin Zubeiry

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments