YANGA YANG’ANG’ANIWA NYUMBANI

Unknown | 9:07 AM | 0 comments


Mashabiki wa Yanga wakiwa hawana matumaini bada ya timu yao kufungwa goli la pili na timu ya Gor Mahia kwenye mchezo wa ufunguzi uwanja wa Taifa

Mashabiki wa Yanga wakiwa hawana matumaini bada ya timu yao kufungwa goli la pili na timu ya Gor Mahia kwenye mchezo wa ufunguzi uwanja wa Taifa
Yanga wameshindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kubanjuliwa na vigogo vya Kenya timu ya Gor Mahia kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kagame Cup uliopigwa leo jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga leo 4
Yanga walitangulia kupata goli dakika ya nne kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao mpya Donald Ngoma walie msajili kutoka klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe lakini bao hilo halikuweza kudumu kwani Haruna Shakava aliisawazishia Gor Mahia goli hilo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana goli 1-1.
Mashabiki wa Gor Mahia wakiwa wanaisapoti timu yao kwa nguvu zote
Mashabiki wa Gor Mahia wakiwa wanaisapoti timu yao kwa nguvu zote
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza baada ya kumpiga kwa makusudi mchezaji wa Gor Mahia.
Mwamuzi wa mchezo SsaliMashood wa Uganda akimwonyesha kadi nyekundu Donald Ngoma
Mwamuzi wa mchezo SsaliMashood wa Uganda akimwonyesha kadi nyekundu Donald Ngoma
Michael Olunga aliifungia Gor Mahia goli la pili dakika ya 45 katika kipindi cha pili na kuipa ushindi timu yake dhidi ya Yanga, mabingwa wa Tanzania bara (Yanga) walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha lakini mambo yalikuwa magumu kwa upande wao.
Kma kawaida ya Yanga na Simba, mashabiki wa Simba wakiiunga mkono timu ya Gor Mahia
Kama kawaida ya Yanga na Simba, mashabiki wa Simba wakiiunga mkono timu ya Gor Mahia
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alikosa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Gor Mahia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa shambulizi lililofanywa na Yanga wakati wakilisakama lango la Gor Mahia wakitafuta goli la kusawazisha.
Msuva akichanja mbuga
Msuva akichanja mbuga
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Yanga Hans van der Pluijm kwa kuwaingiza wachezaji Kpah Sherman akichukua nafasi ya Simon Msuva, Deusi Kaseke akampisha Salumu Telela wakati Joseph Zutah akaingia kumpokea Juma Abdul lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments