RONALDO AWA MWANADAMU WA PILI KUFIKISHA MARAFIKI MILLIONI 100 FACEBOOK

Unknown | 5:30 PM | 0 comments


Real Madrid galactico Cristiano Ronaldo amekuwa mwanadamu wa pili na mwanamichezo wa kwanza kufikisha jumla ya mashabiki million 100 kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Hatua hii inamfanya awe mbele ya Lionel Messi kwa zaidi ya mashabiki million 30.
Nguvu ya kibiashara ya Ronaldo, ambaye pia ana marafiki millioni 30.5 kwenye mtandao wa Twitter, ilionekana wakati alipopost message 6 ndani ya siku mbili akitangaza saa za Tag Heuer.
Messages hizo zilipata hits 34.9 na likes 2.4, thamani ya matangazo hayo ya siku mbili inatajwa kufikia kiasi cha £300,000.
Mchezaji mwenzie Ronaldo wa zamani wa Manchester, Wayne Rooney mapema mwezi huu alikuwa mchezaji wa kwanza wa premier league kufikisha mashabiki 10 kwenye Twitter.
Mwanamuziki Shakira ambaye ni mchumba wa mwanasoka wa FC Barcelona, Gerard Pique ndio alikuwa mwanadamu wa kwanza kufikisha idadi ya mashabiki millioni 100 kwenye mtandao wa Facebook.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments