Baada ya matokeo mabaya – hiki ndicho alichosema Rais wa Simba

Unknown | 10:17 AM | 0 comments

 


IMG_7629.JPGRais Simba, Evans Aveva kwa mara ya kwanza amefungua mdomo wake na kulizungumzia suala la sare mbili katika mechi zao za Ligi Kuu Bara.
Aveva amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kuungana na kuwa pamoja katika kipindi ambacho alikiita hawajapoteza wala kufanya vizuri.
Lakini akaenda mbali zaidi na kusema anamuamini Kocha Patrick Phiri, hivyo wampe muda kidogo kwa kuwa wanapita kwenye kipindi cha mpito. “Hatujafanya vibaya wala kufanya vizuri, sare mbili na hakuna mchezo tuliopoteza. “Ni suala la kujipanga ili kuangalia tutafanya nini katika mechi zinazofuatia. “Uongozi una changamoto nyingi, utaona tulifanya kila linalowezekana kwenye uchaguzi. “Baadaye kwenye usajili, lakini sasa bado mambo hayajakaa vizuri, ni suala la kupambana tu,” alisema Aveva.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments