El Merreikh yatwaa ubingwa Afrika Mashariki

Unknown | 9:51 AM | 0 comments


Kikosi cha El Merreikh
KLABU ya El Merreikh ya Sudan imetwaa ubingwa wa la Afrika Mashariki na Kati, Kombe la kagame jioni ya leo baada ya kuwafunga wenyeji, APR bao 1-0 Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.
Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Alan Wanga aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 24 akimalizia krosi ya Ragi Abdallah.(P.T)
Hilo linakuwa taji la michuano hiyo kwa Merreikh iliyoitoa Azam FC katika Robo Fainali kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0, awali ikibeba taji mwaka 1986 na 1994.
Katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu uliotangulia, Polisi ya hapa iliifunga KCC ya Uganda kwa penalty 4-2 kufuatia sare ya 0-0.
Kwa ushindi huo, El Merreikh wamezawadiwa dola za Kimarekani 30,000 wakati APR, imepata dola 20,000 kwa kushika nafasi ya pili wakati Polisi iliyomaliza nafasi ya tatu imepata dola 10,000.
Chanzo:Bongostaz.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments