VAN GAAL AENDELEZA FURAHA MAN UNITED

Unknown | 4:54 PM | 0 comments


Shinji Kagawa (kushoto), Darren Fletcher (katikati) na Tom Cleverley (kulia), wakishangilia baada ya kuifunga Inter Milan kwa penalti 5 -3.
Fletcher na David De Gea wakishangilia kwa pamoja.
Fletcher akimkumbatia, Michael Kean (kushoto) baada ya ushindi.
David De Gea akipagua moja ya mpira.
Rooney (kulia) akimtoka mchezaji wa Inter Milan.
Hernandez (katikati), Young (kushoto) na Cleverley wakipiga mikwaju ya penalti.
Wilfried Zaha akiwatoka wachezaji wa Inter Milan.
Kocha Louis van Gaal na Msaidizi wake, Ryan Giggs wakifuarahia.
KOCHA Louis van Gaal ameendeleza wimbi la ushindi baada ya Manchester United kuifunga Inter Milan kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 0-0 katika mchezo wa Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa FedEx Field mjini Washington, penalti za United zilitiwa nyavuni na Ashley Young, Javier Hernandez, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Darren Fletcher wakati Marco Andreolli wa Inter aligongesha mwamba. Van Gaal akipanga vikosi viwili, kimoja kila kipindi.
Man United kipindi cha kwanza: Lindegaard, Smalling, Jones, Evans, Valencia, Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney, Welbeck
Kipindi cha pili: De Gea; M Keane, Evans, Blackett; Young, Cleverley, Fletcher, Kagawa, Shaw; Zaha, Nani/Hernandez dk77.
Inter Milan: Handanovic/Carrizo dk63, Ranocchia, Vidic/Andreolli dk72, Juan Jesus, D'Ambrosio, Jonathan, Kuzmanovic/Laxalt dk63, Krhin/M'Vila dk46, Dodo/Nagatomo dk63, Botta/Taider dk63 na Icardi.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments