YAYA TOURE: SITAMBULIKI KWA KUWA NI MUAFRIKA

Unknown | 12:32 PM | 0 comments


yaya_hatari_e8c16.jpg
Na Riziki Mashaka.
Mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast ambaye pia anaichezea klabu ya Manchester City, Yaya Toure amesema kuwa asili yake ya uafrika ni kigezo kikubwa kinacho mfanya ashindwe kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Toure alisema kuwa mashabiki wengi wa ulaya hususan ni uingereza hawamthamini sana kwa kuwa ni muafrika.
Akiongea na City Tv, Toure alisema ''ukija Afrika ukiuliza jina Messi kila mtu atakwambia anamjua lakini ukienda ulaya na kuuliza jina Yaya Toure watu watakuuliza, Yaya Toure ni nani? Hali hii inaonesha kuwepo kwa ubaguzi wa hali ya juu katika soka la ualaya, alisema Yaya.
Baada ya kunyakua kombe cha Capital One katika dimba la Wembley mnamo mwezi Machi, mchezaji Samir Nasri ambaye pia ni kiungo wa Manchester City alisema ''Yaya Toure ni mchezaji ambaye anastahili kuwa kiungo bora wa dunia kama asingekuwa muafrika'' kauli hiyo ya Nasri iliungwa mkono na kiungo huyo raia wa Ivory Coast '' nafikiri alichokisema Nasri ni kweli kabisa'' Yaya Toure aliwaambia waandishi wa habari wa bbc.
Yaya Toure ni mmoja kati ya wachezaji sita waliochaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika soka la Uingereza maarufu kama '' Professional Footballers' Association (PFA)'' ambapo atashindana na miamba mingine kama Steven Gerrard, Daniel Sturridge and Luis Suarez, Eden Hazard and Adam Lallana na mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa Aprili 27.
Toure amewahi kushinda vikombe vya ligi akiwa Uispaniola, Uingereza na Ugiriki pia aliwahi kunyakua kombe la mabingwa ulaya akiwa na Barcelona.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments