MOURINHO: NIACHIENI CHELSEA YANGU, KIKOSI SUBIRINI JUMAPILI

Unknown | 11:41 PM | 0 comments


395300_heroa
JOSE Mourinho amegoma kuzungumzia kuhusu kikosi atakachopanga katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England baina ya klabu ya Chelsea dhidi ya Liverpool jumapili ya wiki hii katika dimba la Anfield.
Siku za karibuni, Mreno huyo alikaririwa akisema atapanga kikosi dhaifu katika mechi hiyo ili kuwapumzisha wachezaji wake nyota kuelea nusu fainali ya pili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Atlectico Madrid jumatano ya wiki ijayo uwanja wa Stamford Bridge.

Mourinho alipoulizwa kuwa anaidharau ligi ya England mpaka apange kikosi dhaifu?, kocha huyo, 51, alisema mambo ya timu yake aachiwe yeye.
“Siku zote kuchagua kikosi kitakachocheza ni siri ya kocha, Kama mtu anauliza swali hilo, siwezi kumjibu”.
“Kitu cha msingi ni klabu yangu na mashabiki wetu. Nahita
ji kuilinda klabu na mashabiki wa Chelsea”.
“Kama hatusaidiwi kutimiza ndoto zetu na malengo yetu, basi kuna sababu ya kutuacha tufanye mambo yetu. Subirini jumapili na mtajua timu itakayocheza” Alisema Mourinho.
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid alipoulizwa kama mashabiki wa Chelsea watafurahishwa na mabadiliko ya kikosi, alijibu kuwa mashabiki wa Stamford Bridge watakuwa na imani na maamuzi.
Mourinho alieleza kuwa leo hii hakuwa huru katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia adhabu aliyopewa na chama cha soka cha England, FA baada ya kumpongeza mwamuzi Mike Dean aliechezesha mechi ya Chelsea dhidi ya Sunderland na kushuhudia paka weusi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
FA wameyachukuliwa maneno ya Mourinho kama kejeli, lakini yeye anachukuliwa kivingine.
Aliongeza: “Kila ninapozungumza kuna madhara, hata kama nikisema mwamuzi amefanya kazi nzuri napewa adhabu, kwahiyo sina uhuru kabisa. Kama mnataka mkutano mzuri nendeni mkazungumze na FA na sio mimi”.
Pia Mourinho amethibitsiha kuwa nahodha wake John Terry na mshambuliaji wake Eden Hazard watakosa mechi ya jumapili na wapo hatarini kuwakosa Atletico jumatano.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments