CHICHARITO AMWAMBIA MOYES ANATAKA KUONDOKA

Unknown | 8:20 AM | 0 comments


UVUMILIVU umemshinda mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Javier Harnandez `Chicharito` na sasa ameitaka klabu yake kumuuza majira ya kiangazi mwaka huu baada ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.
Chicharito ameongea mara tatu na bosi wake David Moyes katika miezi miwili iliyopita juu ya yeye kunyimwa nafasi ya kucheza, huku akianzishwa katika mechi tano tu za ligi kuu msimu huu.
Nyota huyo raia wa Mexico ameiambia klabu yake kuwa atasikiliza ofa zikazokuja juu yake majira ya joto na hadhani kama yupo katika mipango ya Moyes hapo baadaye.
Chicharito ameshindwa kupata namba ya kudumu mbele ya Wayne Mark Rooney, Robin Van Persie na Danny Welbeck.
Sasa mshambuliaji huyo amefikia maamuzi ya kuondoka huku akihusishwa na mpango wa kuhamia Atletico Madrid kama mrithi wa Diego Costa mwenye kila dalili ya kujiunga na Chelsea majira ya kiangazi.
Chicharito mwenye miaka 25 alihuzunishwa baada ya kukosa nafasi ya kuanza kwenye mechi ya robo fainali ya UEFA dhidi ya Bayern Munich, huku kocha Moyes akimuanzisha Rooney ambaye hakuwa fiti kwa mechi ile.
Siku nne Kabla ya kuwakabili Bayern, Chicharito alicheza dakika 90 katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Newcastle ambapo walishinda 4-0, hivyo alijiona kuwa anastahili kuanza katika kikosi cha Man United kwa kuzingatia kiwango chake kwenye mechi ile na mazoezi ya kujiandaa na safari ya Allianz Arena.
Msimu huu, mshambuliaji huyu amecheza mechi 31 katika mashindano yote, na ameanzia benchi kwenye mechi 20, huku akifunga mabao 9 katika msimu huu mgumu kwa David Moyes.

Nahodha wa Man United, Nemanja Vidic naye yuko mbioni kujiunga na Inter Milan, wakati huo huo Rio Ferdinand, Patrice Evra, Shinji Kagawa, Nani, Anderson na Alex Buttner ni miongoni mwa wachezaji wengi wanaotarajiwa kuondoka Old Traffo

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments