ARSENAL YAKUNG'UTWA 3-0 NA EVERTON ENGLAND
KWELI
ngoma ya kitoto haikeshi. Arsenal imekung'utwa mabao 3-0 na Everton
Uwanja wa Goodison Park na kuzidi kujitoa kwenye mbio za ubingwa.
Mabao
yaliyoizamisha timu ya Arsene Wenger leo yamefungwa na Steven Naismith,
Romelu Lukaku na Mikel Arteta aliyejifunga na sasa The Gunners
inafikisha mechi 33 za kucheza, lakini inabaki na pointi zake 64.
Category: uingereza



0 comments