YANGA YACHEZEA VIRUNGU VYA MGAMBO ... MBEYA CITY YAITUNGUA PRISONS
![]() |
MGAMBO |
Yanga wamekiona cha moto baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Mgambo Shooting mjini Tanga.
Wakati Yanga wanapoteza dhidi ya Mgambo, Mbeya City wameendelea na ushindi kwa kuibuka na ushindi kwenye Mbeya derby kwa kuichapa Prisons bao 1-0.
Yanga wameshindwa kifunga Mgambo Shooting licha ya kuwa na wachezaji pungufu baada ya beki wake, Mohammed Neto kulambwa kadi nyekundu.
Katika mechi hiyo ya vutanikuvute kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Yanga ilishambulia sana huku mipira zaidi ya mitatu ikigonga mwamba lakini iliambulia kipigo.
Mgambo walianza kufunga bao kupitia kwa Fuli Maganga lakini Yanga wakasawazisha kupitia Nadir Cannavaro kwa penalti.
Lakini Mgambo wakaongeza la pili kwa penalti Bamili Busunzu.
Lakini Mgambo wakaongeza la pili kwa penalti Bamili Busunzu.
Bao pekee la la Mbeya City lilifungwa na Paul Nonga na jitihada za Prisons kutaka kusawazisha hazikuzaa matunda.
Category: tanzania
0 comments