YANGA WAPATA AJALI YA BASI MIKESE, MKOANI MOROGORO

Unknown | 10:00 PM | 0 comments

 
Hatari; Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm akiruka dirishani kutoka kwenye basi la timu hiyo baada ya kunusurika kupinduka asubuhi ya leo eneo la Mikese, Morogoro wakati wakijaribu kukwepa basi la abiria. Yanga SC ilikuwa inatokea Morogoro ambako jana ilicheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar na kutoka sare ya bila kufungana.
Basi la Yanga likiwa limeinama upande mmoja baada ya kukwepa basi la abiria. Hakuna aliyeumia na timu imeendelea na safari ya kurejea Dar es Salaam baada ya mkasa huo


Tumepata ajali mzee; Kocha Pluijm kulia akiozungumza na simu na kushoto kwake ni kocha wa makipa, Juma Pondamali



Wachezaji wakitokea madirishani kuokoa maisha yao baada ya kunusurika ajali mbaya asubuhi ya leo Mikese

PICHA ZOTE KWA HISANI YA BLOG YA BIN ZUBEIRY

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments