MOURINHO YUPO TAYARI KUIFUNDISHA UNITED HATA LEO KAMA MOYES AKIFUKUZWA
Kuonyesha heshima anapokutana nayo
Achana na ile mara ya kwanza alipokuwa Porto, tangu Mourinho
alipoondoka England mara ya kwanza, amekuwa akiizungumza vizuri United
na kuonyesha heshima kubwa kwa Ferguson tofauti na makocha wengine.
Wakati
alipokuwa Madrid, siku timu yake ilipocheza dhidi ya United, Mourinho
alionekana kuwa mwenye nidhamu kubwa tofauti na awapo uwanjani wakati
timu yake ikicheza dhidi ya timu nyingine.
Hata mara baada ya mechi hiyo ambayo Madrid ilishinda, alisema: "Timu bora imepoteza mchezo.”
Kumtetea Alex Ferguson
Wakati Ferguson alipomweka benchi straika wake tegemeo, Wayne Rooney,
katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, Mourinho alisema: "Sir
Alex ameshinda kwa kufanya maamuzi mengi magumu, kila anachofanya yupo
sawa na haihitaji maswali, ni kocha aliyetengeneza historia."
Kuitetea United ilipoyumba
Mwanzoni mwa msimu huu, United ilikuwa ikiyumba kama ilivyo sasa,
haikupata matokeo mazuri, lakini Mourinho alipoulizwa alisema: “United
ni United, inaweza kufanya lolote na muda wowote.”
United bado ni timu kubwa
Mourinho yupo Chelsea, ni timu kubwa lakini kwa sifa na rekodi za ubora
bado haijafikia kuwa daraja moja sawa na AC Milan, Barcelona,
Liverpool, Real Madrid, Juventus na Inter Milan, hivyo nafasi hiyo ni
kubwa.
Heshima kila anapocheza dhidi ya United
Mara kadhaa
imewashangaza wengi kuwa Mourinho anapocheza dhidi ya timu kubwa
nyingine ni jambo la kawaida kukwaruzana na wapinzani, iwe wachezaji au
makocha, lakini anapofika Old Trafford huwa anaonyesha heshima na kuwa
mstaarabu.
Hana maneno ya ‘shombo’ akikutana na Mashetani hao,
lakini mara nyingi amekwaruzana na mabosi wa timu nyingine kama vile
Manchester City na Arsenal.
Kujulishwa na Ferguson kinachoendelea
Hivi karibuni Mourinho alisema mara baada ya United kufanya maamuzi ya
kumchukua Moyes, alipata taarifa hizo mapema kutoka kwa Ferguson
mwenyewe, wengi wanajiuliza kwa nini kocha huyo mkongwe alienda
kumjulisha! Wanaamini kuna ukaribu zaidi ya urafiki juu ya taarifa hizo.
Katika kura za maoni zilizopigwa kwenye mitandao barani Ulaya
zinaonyesha kuwa mashabiki wengi wa United wamekubali hoja kuwa United
ingemchagua Mourinho kuliko Moyes.
Category: uingereza
0 comments