BALE KUTUMIA `NJUMU` MPYA KESHO KUWAKABILI Schalke 04

Unknown | 10:42 PM | 0 comments

New wheels: Gareth Bale is looking forward to wearing his new adidas crazylight boots

Viatu vipya: Gareth Bale atavaa viatu vyake vipya kutoka kampuni ya adidas
Bonkers: The garish green and black arrow design is certain to send defenders crazy
Jinsi viatu hivyo vilivyobuniwa, lazima mabeki wachanganyikiwe
MCHEZAJI ghali zaidi duniani, Gareth Bale kesho katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Schalke 04 dimba la Santiago Bernabeu atavaa viatu vipya `njumu` kutoka kampuni ya Adidas.
Viatu hivyo vya `adidas F50 crazylight`, vina uzito wa gramu 135 na vimebuniwa kwa ufundi mkubwa.
Gareth Bale alionekana leo hii akijaribu viatu hivyo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mazoezi ya Real Madrid na atakuwa wa kwanza pekee kuvaa viatu hivyo.
Nyota huyo raia wa Wales atavitumia kesho dhidi ya
Schalke uwanja wa Bernabeu.
"Nimevijaribu viatu hivi kwenye mazoezi na nimejisikia vizuri". Alisema Bale ambaye ameandika kwenye akaunti yake ya Twita kuwa atatumia viatu vipya.
"Ni viatu vyepesi sana na vitanipa faida kubwa katika uchezaji wangu". Alisema

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments