JOHN TERRY AIOKOA CHELSEA ENGLAND
BAO
 la dakika ya mwisho kabisa la Nahodha aliyerejea John Terry limeipa 
Chelsea ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Everton jioni hii katika Ligi Kuu ya
 England.
Ilikuwa
 kama Jose Mourinho tayari amekwishapoteza pointi mbili katika mbio za 
ubingwa kutokana na timu hizo kuwa hazijafungana hadi Phil Jagielka 
alipomchezea rafu Ramires.
Frank
 Lampard akaenda kupiga mpira wa adhabu  ambao uliguswa na Branislav 
Ivanovic na Terry akateleza kwenda kuusukumia nyavuni dhidi ya kipa Tim 
Howard.
Baada
 ya ushindi huo wa mbinde unaoifanya Chelsea itimize pointi 60 baada ya 
mechi 27 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, na The Blues watasafiri hadi 
Galatasaray kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Hatua ya 16 Bora 
Jumatano.

Mkombozi: Frank Lampard (kushoto) na John Terry ushirikiano wao umeipa bao la ushindi Chelsea

John Terry alikuwa wa kwanza kuugusa mpira huku Slyvain Distin, Leighton Baines na Phil Jagielka wakiangalia

John Terry akiteleza kufunga dhidi ya Tim Howard 
Category: uingereza


0 comments