CHELSEA 1-1 NA GALATASARAY ULAYA
CHELSEA
imepata sare ya ugenini ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Galatasaray
katika mchezo wa kwanza wa 16 Bora Ligi ya Mabingwa Bora Ulaya usiku
huu.
Fernando
Torres alitangulia kuifungia The Blues dakika ya tisa na kuifanya
Chesea kuwa timu ya kwanza ya England kufunga bao katika 16 ya Ligi ya
Mabingwa msimu huu, baada ya wiki iliyopita Arsenal kufungwa 2-0 na
Bayern Munich na Manchester City kufungwa 2-0 na Barcelona, wakati jana
Manchester United iIifungwa 2-0 pia ugenini na Olympiacos.
Hata hivyo, wenyeji Galatasaray walisawazisha bao hilo dakika ya 64 kupitia kwa Chedjou.
Hatufungwi sisi; Fernando Torres akishangilia na wenzake baada ya kuifungia bao Chelsea usiku huu |
Kitaalamu: Fernando Torres akiifungia bao la kuongoza Chelsea
Category: uingereza
0 comments