BAADA YA KUTUMIA FEDHA YOTE YA BALE - SPURS WANAANZA KUONA NDOTO YAO YA KUCHEZA CHAMPIONS LEAGUE IKIPOTEA - TAKWIMU ZINAONYESHA EUROPA LEAGUE INAUWAMIZA
Katika
miaka ya hivi karibuni klabu ya Tottenham imekuwa ikjaribu kwa kila
hali kuweza kumaliza katika nafasi nne za juu za msimamo wa ligi kuu ya
England, ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kucheza kwenye michuano ya
klabu bingwa ya ulaya. Pamoja na jitihada zote lakini wameshindwa
kufikia malengo.
Msimu
huu kama ilivyo misimu kadhaa iliyopita Tottenham wanaonekana kabisa
hatma yao itabaki katika kucheza michuano ya Europa, hasa baada ya
kipigo cha jana kutoka kwa Norwich.
Kuna
pengo la pointi sita baina yao na Liverpool ambao wanashika nafasi ya
nne na pia wamepitwa kwa namba kubwa ya tofauti ya mabao.
Zaidi
ya £100million zimetumika katika kununua wachezaji, kubadili kocha,
lakini hali bado inaonekana kuwa ile ile ya miaka yote.
Ikiwa
watashindwa kuingia top 4 itakuwa sahihi hata kwa wale viongozi wa juu
nao wajiangalie, maana kama watabaki nafasi ya tano wataishia kwenye
Europa League kama msimu uliopita.
Ushiriki
wa timu katika michuano ya Europa umekuwa moja ya sababu klabu hii
kushindwa kupenya katika kundi la timu za juu katika Epl.
Kocha
wao Tim Sherwood anakataa kwamba kufungwa kwao kwenye dimba la Carrow
Road chanzo chake kimeanzia huko Ukraine walipotoka kucheza mechi ya
Europa Alhamisi wiki iliyopita. Lakini hii ni mara ya tano msimu huu
Spurs wanafungwa siku chache baada ya kucheza katika Europa League,
vipigo ambavyo vimeifanya kufikisha jumla ya vipigo saba kwenye ligi.
‘Ilikuwa
kama kufungwa mechi nyingine tu' hivi ndivyo kocha wa Spurs
alivyoelezea kipigo cha 1-0 dhidi ya Dnipropetrovsk lakini kusafiri kwa
safari ya umbali wa 3,000-mile baina ya siku ya Alhamisi na Jumapili ni
sababu nyingine ya kufanya kwao vibaya kutokana na uchovu.
Hali
huwa hivyo pia kwa timu zinazocheza Champions League katika safari
ndani ya bara la ulaya, lakini michuano ya ulaya mechi zake zinachezwa
baina ya Jumanne na Jumatano, ikimaanisha kwamba kuna nafasi ya
kupumzika siku 3 au mbili - muda mwingine zaidi.
Utafiti
uliofanywa na kocha wa kidachi Raymond Verheijen mnamo mwezi May 2012
uliangalia matokeo ya mechi 27,000 ndani ya bara la ulaya na kugundua
kwamba timu ambazo zinacheza baada ya siku mbili baada ya mapumziko
dhidi ya ambazo zinakuwa na mapumziko ya angalau siku tatu - zilionekana
kuwa na 39% ya kushinda nyumbani na 42% ya kupoteza ugenini.
Kwa
timu zinazocheza katika Europa League, utafiti huu unawagusa zaidi.
Baada ya mechi ya Alhamisi usiku, Jumapili ndio hucheza mechi yao ya
ligi hasa katika EPL, lakini bwana Verheijen anasema Jumatatu ingefaa
zaidi badala ya jumapili.
Sherwood
anataka taji katika CV yake, hivyo ni jambo la kueleweka anataka
kushinda kombe la Europa. Lakini, mashindano haya kwa hakika yanakuwa
kizingiti kwenye kiwango cha mechi za ligi.
Mashabiki
wa Spurs, na mwenyekiti Daniel Levy, wanaweza wakakutana na hali ile
ile waliyokutana nayo siku ya mwisho ya ligi kma msimu uliopita.
Jinamizi la Europa league linawamaliza Spurs.
Category: uingereza
0 comments