THE 11+ –PROGRAMU YA KUZUIA AU KUEPUSHA MAJERAHA MICHEZONI/SOKA
Pengine Umewahi
kusikia mtu ambaye amewahi kuumia . Mchezo wa soka ni mchezo ambao una hatari
ya kumletea majeraha mtu anayecheza. Lakini habari njema ni kwamba utafiti wa kisayansi
umeonyesha kuwa matukio ya kuumia katika soka kunaweza kupunguzwa kwa progammu
maalum za kuzuia majeraha kwa wachezaji.
11 ni proggramu rahisi
na yenye kutumia muda mfupi ya kumuepusha au kumkinga mchezaji na majeraha
ambayo inajumuisha mazoezi kumi ambayo yana ushahidi unaoonyesha jinsi
inavyofanya kazi.
11 ni progranu inayolenga kuongeza uungwana yaani FAIR PLAY
latika mchezo na haihitaji kitu kingine cha ziada zaidi ya mpira na inafanywa
kwa muda usiopungua dakika 10 mpaka 15 . Programu hii ni ya uhakika kuliko mazoezi
mengi ambayo wachezaji huyatumia na inaweza kutumika katika nafasi ya mazoezi
mengine.
Mazoezi yaliyopo
katika programu hii yamejikita kwenye mbinu maalum za ambazo makocha wanapaswa
kujifunza na kuzizoea ili waweze kuwapa wachezaji ili waweze kujenga misuli
hasa ya mapaja pamoja na kumudu mnyumbuliko wa misuli kuendana na kasi ya
mchezo.
Moja ya mazoezi haya ni jinsi ya kujenga misuli kunyooka na kuwa
thabiti.
Kanuni na programu hii
ya 11 inatakiwa kufanywa kila siku katika wakati wa mazoezi ya wachezaji hasa
baada ya kupasha mwili moto na kunyoosha misuli . Ili kuhakilisha uhakika wa
mazoezi haya yanatakiwa kufanywa kama
inavyotakiwa bila kukosea na kabla ya mechi unapaswa kuyafanya mazoezi haya kwa
ufupi ili misuli isikakamae.
Programu hii
ilianzishwa na kuendelezwa na FIFA katika idara yake ya afya na utafiti kwa
ushirikiano na kundi la wataalamu wa kimataifa wa masuala ya afya michezoni .
Baada ya kufuata programmu hii mchezaji ataongeza kiwango chake cha kuperform
na kupunguza uwezekano wa kupata majeraha .
Category: tanzania
0 comments