PIGO ARSENAL NA ENGLAND, WALCOTT NJE MIEZI SITA...ATAKOSA HADI KOMBE LA DUNIA

Unknown | 7:59 AM | 0 comments

 

TIMU ya taifa ya England na Arsenal zimepata pigo kubwa baada ya Theo Walcott kutakiwa kuwa nje kwa kipindi chote kilichobaki cha msimu pamoja na Kombe la Dunia, baada ya kuumia goti.
Winga huyo alitolewa nje Jumamosi katika mechi ya Kombe la FA Arsenal ikiifunga Tottenham baada ya kuumia na baada ya vipimo anatakiwa kuwa nje kwa mzi sita kwa sababu ya maumivu ya goti la mguu wa kushoto.
Habari hizo hakika ni pigo kubwa kwa kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson kuelekea Fainali za Kombe la Dunia katikati ya mwaka huu nchini Brazil.
Maumivu: Theo Walcott anatakiwa kuwa nje kwa miezi sita baada ya kuumia goti la mguu wa kulia
Clash: Walcott (left) sustained the injury in this challenge with Tottenham's Danny Rose
Alivyoumia: Walcott (kushoto) alipata maumivu hapa wakati anapambana kugombea mpira na Danny Rose wa Spurs
Blow: Walcott (left) will be out for the rest of Arsenal's season and England's World Cup bid
Walcott (kushoto) sasa atakuwa nje kwa kipindi chote cha msimu kilichobaki na atakosekana pia kwenye kikosi cha England Kombe la Dunia
Credit: Bin Zubeiry

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments