MAMBO YA YANGA HAYO UTURUKI ... LEO DIMBANI KUWAVAA ANKARA SEKER SPOR.

Unknown | 7:33 AM | 0 comments

 
Wakati mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Yanga Leso wanacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya timu daraja la kwanza ya Ankara Seker Spor, uongozi wa timu hiyo jana utatangaza jina la kocha mkuu katika mkutano na waandishi wa habari.
Mechi hiyo itachezwa saa 9.00 za Tanzania kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mashindano wa kimataifa wa Yanga, Seif “Magari” Ahmed amesema kuwa mazoezi ya jana yalifanyika asubuhi kutokana na jua kuwahi kuzama na hali ya hewa kubadilika.
Ahmed alisema kuwa wachezaji wanaendelea vizuri na mpaka sasa wamepania kufanya vyema katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.



Alisema kuwa baada ya mechi hiyo, timu hiyo itaendelea na mazoezi kabla ya kucheza mechi nyingine mbili na timu za madaraja ya juu.
“Timu imeanza kambi rasmi, na mazoezi mazuri na maandalizi yametupa moyo japo ka siku ya kwanza, watacheza mechi ya kirafiki ya kwanza na timu ya daraja la kwanza, n mechi nzuri kwani timu hiyo inashika nafasi za juu katika ligi hiyo,” alisema Seif.
Alisema kuwa kwa sasa timu yao inakaa mji mwingine tofauti na Antalya ambao upo kilometa 70 kutoka mji wao wa zamani. Wamefikia hotel ya ufukweni ijulikanayo wa jina la Suino Beach Hotel and Site ambayo ina hadhi ya kimataifa.



Wakati huo huo;  uongozi wa klabu hiyo kesho utamtambulisha kocha mkuu wa klabu hiyo katika mkutano maalum na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo.
Seif alisema kuwa wamepitisha majina matano na walikuwa kwenye makubaliano nao mmoja wao ambaye jana tutamtangaza rasmi.
Alisema kuwa wamepata kocha mzuri ambaye anajua mazingira ya Afrika na anajua maisha ya mpira kwa bara hili.
Beki wa kushoto wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Robert Carlos leo asubuhi  amekutana na wachezaji na viongozi wa Yanga kabla ya mazoezi.

Carlos Kwa sasa ni kocha wa timu ya Sivasspor iliyopo Ligi Kuu nchini Uturuki, Yanga pamoja na Sivasspor zimeweka kambi kwenye hotel ya Sueno Beach zikijiandaa na mashindano mbali mbali yanazikabil,Yanga wakiwa wameweka kambi kujiandaa na raundi ya pili ya ligi kuu ya Vodacom wenzao Sivasspor wanajiandaa na mchezo kombe la chama cha soka nchini humo ambao utachezwa siku ya jumanne.
Roberto Carlos akiwa na wachezaji wa Yanga nchini Uturuki.

    Nizar Khalfan na kocha Charles Boniface Mkwasa wakiwa na Roberto Carlos nchini Uturuki.
Roberto Carlos akiwa na Baraka Kizuguto pamoja na Juma Pondamali.

 IMEANDALIWA NA BARAKA KIZUGUTO

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments