MAKOCHA WAPEWA LESENI B NA WAKABIDHIWA VYETI
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine
amekabidhi leseni B kwa makocha walioshiriki kozi iliyofanyika mjini
Zanzibar mwaka jana.
Jamhuri
Kihwelo alipokea leseni hiyo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) kwa niaba ya washiriki wengine tisa waliofuzu mafunzo
hayo.
Makocha
wengine waliofuzu kozi hiyo iliyoendeshwa na mkufunzi Bhekisisa Boy
Mkhonta kutoka Swaziland ni Abdulghan Msoma, Hafidh Badru, Nasra Juma
Mohamed, Gulam Abdallah Rashid, Mohamed Ayoub Suleiman, Shaaban
Ramadhan, John Simkoko na Hemed Suleiman Ali.
Hivi
sasa Tanzania ina makocha 40 wenye leseni B za CAF baada ya wengine 31
kufuzu katika mafunzo yaliyofanyika mapema mwaka juzi jijini Dar es
Salaam chini ya mkufunzi Honor Janza kutoka Zambia.
Category: tanzania
0 comments