KCC WABEBA KOMBE LA MAPINDUZI BAADA YA KUMRARUA SIMBA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Nahodha wa timu ya KCC ya Uganda, Kawooya Fahad, Kombe la Mapinduzi baada kumalizika kwa mchezo wa Fainali wa Kombe la Mapinduzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo jioni. Katika mchezo huo KCC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa katika dakika ya 7 ya mchezo.
Baada ya bao hilo dakika mbili baadaye Kocha wa Simba, Logalusic, alianza kufanya mabadiliko kwa kumtoa beki Haruna Shamte na kumuingiza William Lucian, na dakika ya 29, alimtoa Awadh Juma na kumuingiza Ramadhan Chombo, na kumtoa Haruna Chanongo na kumuingiza Betram Mwombeki na baadaye tena alimtoa beki, Issa Rashid na kumuingiza Uhuru Seleman. Pamoja na mabadiliko hayo bado hayakuweza kuzaa matunda na kubadilisha matokeo hivyo hadi mwisho wa mchwzo KCC 1 Simba 0.
Meza kuu ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar.. na baadhi ya viongozi.
Manahodha wa timu hizo, Amri Kiemba na Kawooya Fahad, wakichuana kuwania mpira.
Ramadhan Singano wa Simba akichuana na Magoola Omar.
Sehemu ya mashabiki na viongozi wa waliohudhuria mtanange huo.
Sehemu ya mashabiki wa Simba waliohudhuria mtanange huo.
Mwenyekiti wa Simba 'Anayeshinikizwa kuachia madaraka' Aden Ismail Rage, (wa tatu kuli mbele) akiwa ni mmoja kati ya waliohudhuria mtanange huo.
Kocha wa Simba, Lugalusic, akitoa maelekezo kwa beki wake Joseph Owino.
Kocha akiendelea kutoa maelekezo......
Mshambuliaji wa Simba Amis Tambwe, akijikunja kupiga mpira wa kichwa.
Mabeki wa Simba Issa Rashid (kulia) na Joseph Owino, wakimdibiti mshambuliaji wa KCC, Odur Tony.
Kocha wa Simba, Logalusic akiwapa Big Up wachezaji wa KCC baada ya mchezo huo kumalizika.
credit: Sufiani mafoto blog
Category: tanzania
0 comments