HII KALI NA INALEWESHA ... MCHEZAJI AFANYA MAZOEZI NA SKETI NCHINI USKOCHI
![]()  | 
Partick Thistle huenda ikawa ni 
klabu ambayo inapokuwa uwanjani haina la kushangaza lakini huku nyuma ya
 pazia inapokuwa katika uwanja wake wa mazoezi vituko ni sehemu ya 
kufurahisha ndani ya  klabu hiyo ya Uskochi.
Kiungo Gary Fraser mwenye umri wa 
miaka 19 akiwa mazoezini alivalia kivazi cha kufungia mwaka cha rangi ya
 pinki ambacho kimeunganishwa na sketi iliyokuwa katika rangi moja.
Fraser kwasasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Bolton Wandarers ya Uskochi.
Inadhaniwa kuwa Fraser 
alivalia kivazi hicho akijitofautisha na wenzake kutokana na kwamba 
alikuwa mkosefu licha ya kwamba alipokea madharau kutoka kwa wenzake 
huku wengine wakidhihaki vazi lake.
Fraser bado yuko kwa mkopo katika 
klabu hiyo akitokea katika klabu ya Bolton Wanderers, na alikumbana na 
adhabu ya kusimama michezo nane baada ya kushambuliana na mchezaji 
mwenzake wa Under-20 katika mchezo dhidi ya Dunfermline.
Fraser
 anarejea kutoka kifungoni siku ya mwaka mpya ambapo watakuwa wakielekea
 kucheza dhidi ya Celtic, na inadhaniwa kuwa Thistle huenda akaongeza 
kipindi chake cha mkopo mpaka mwisho wa msimu.
Kitu kizuri kwa Fraser ni kwamab 
angalau katika kivazi chake hicho mguuni alivalia viatu vyeusi tofauti 
na hali ilivyo siku hizi hususani katika soka la England ambapo 
wachezaji wamekuwa na tabia ya kuvaa viatu vya marangi mengi.

Begani akilia: Fraser akifarijiwa na mchezaji mwenzake James Craigen (kushoto) wakati wa mazoezi 
Fraser (kulia) alifungiwa kwa mchezo mbaya wa michuano ya Under-20 dhidi ya Dunfermline
Category: uingereza



0 comments