FIFA yahamisha muda wa kombe la dunia 2022 huko QATAR.
Baada
ya utafiti wa muda mrefu na majadiliano yaliyochukua zaidi ya mwaka
mmoja shirikisho la soka ulimwenguni limefikia uamuzi wa kutofanyika kwa
mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka 2022 katika kipindi cha msimu wa
kiangazi .
Kwa
mujibu wa katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke michezo ya kombe la dunia
haiwezi kufanyika kwa msimu huo nchini Qatar kutokana na hali ya hewa
kuwa joto kali na hivyo kuhatarisha afya na usalama wa wachezaji.
Kwa
muda mrefu FIFA imekuwa ikifanya utafiti kufuatia malalamiko
yaliyotolewa na baadhi ya mataifa kuhusiana na ugumu wa michezo ya kombe
la dunia kufanyika nchini Qatar wakati wa msimu wa kiangazi ambapo hali
ya hewa ni nyuzi joto 38 mpaka 40 mazingira ambayo hayawezi kutumika
kwa mechi za soka hasa kwa timu za ulaya .
FIFA
imetangaza kuwa mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka 2022 yatafanyika
kati ya Novemba tarehe 15 na January 15 katika wakati ambao msimu
utakuwa wa baridi.
Maamuzi
haya yatazua utata miongoni mwa wadau na wadhamini wa Mashindano haya
ikiwemo kampuni ya Fox Sports ya Marekani ambayo imeingia mkataba na
FIFA wa kurusha matangazo ya michezo ya kombe la dunia katika msimu wa
joto huku wakiwa na mikataba ya kurusha matangazo ya michezo mingine
katika msimu wa baridi.
Category: uingereza
0 comments