YANGA YAMTEMA RASMI BRANDTS
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano Abdallah Bin Kleb (katikati) akiongea na
waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto ni Musa
Katabaro na kulia Afisa Habari Baraka Kiziuguto. Picha kwa Hisani ya
Young Africans Official Website
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
KIMENUKA
jangwani!. Siku mbili tu baada ya Yanga kupata kipigo cha mabao 3-1
kutoka kwa Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe, uongozi wa klabu
hiyo umetangaza kuachana na kocha wake, Mholanzi, Ernie Brandts.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema
Uongozi umempatia taarifa (Notice) ya siku thelathini (30) , Brandts
juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Bin
Kleb amesema maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika
michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe
dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
“Hatua
ya Yanga kusitisha mkataba na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni
moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze
kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili”. Alisema Bin
Kleb.
Bin
kleb aliongeza kuwa Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC
na wapinzani wao Simba Sc, na soka walilocheza kwenye mechi ya Nani
Mtani Jembe ni dhahiri kocha amefikia mwisho kimbinu na hana njia
mbadala.
“Yanga
imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali
iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza
pointi”. Alisema Bin Kleb.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua
mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa
moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.
Bin
kleb aliongeza kuwa Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na
mazoezi kama kawaida kila siku asubuhi katika uwanja wa bora
kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya
kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.
“Ili
kuhakikisha timuYanga inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha
maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote
zitakapokamilika tutawajulisha”. Alisema Bin Kleb.
Ernie Brandts amepewa `Notice` ya kusitishwa kwa mkataba wake.
Aidha
uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye
ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na
Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
“Tunawaomba
wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia
matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha
timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika
mzunguko wa pili wa VPL”. Alisema Bin Kleb.
Katika hatua nyingine , Bin Kleb amethibitisha ushiriki wa Yanga katika Kombe la Mapinduzi Januari mwakani visiwani Zanzibar.
Mwaka huu Yanga haikushiriki kombe la mapinduzi kufuatia kuwa na ziara nchini Uturuki ambako iliweka kambi ya wiki mbili.
Category: tanzania
0 comments