TANZANITE YAKUBALI KICHAPO CHA MABAO 4-1 DHIDI YA WATOTO WA MANDELA
Mshambuliaji
 wa Tanzanite, Shelda Boniface (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa 
Afrika ya Kusini, Meagan Newman, wakaati wa mchezo wa kuwania kufuzu 
kucheza michuano ya Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya umri wa miaka 
20, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalm, leo jioni. 
Katika mchezo huo Afrika ya Kusini ilishinda mabao 4-1. 
*********************************************
 TIMU
 ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ya Tanzania 'Tanzanite' leo 
imefungwa jumla ya mabao 4-1 na Afrika Kusini 'Basetsana' kwenye mchezo 
wa raundi ya pili ya  kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani 
nchini Canada kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Afrika
 Kusini ilianza vyema mchezo huo kwa  kuwazidi  ujanja Tanzanite katika 
kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya kuzitumia vizuri nafasi 
walizopata kwa kufunga bao la kwanza dakika ya nne ya kipindi cha kwanza
 kupitia kwa mchezaji wake Amogelang Motay.
Bao
 hilo liliamsha mashambulizi  makali kwa Tanzanite waliokuwa wakitafuta 
nafasi ya kusawazisha ambapo dakika ya 13 walifanikiwa kusawazisha 
kupitia kwa Theresa Yohana aliyepiga shuti kali la mita kama 30 na 
kumwacha kipa wa Afrika ya Kusini akiduwaa.

Mashambulizi
 yaliendelea pande zote mbili, ambapo dakika ya 17 mchezaji wa Afrika 
Kusini Shiwe Nogwanya, aliipatia timu yake bao la pili lililodumu hadi 
mapumziko.
Baada
 ya mapumziko timu zote zilikuwa zikifanya mashambulizi  lakini Afrika 
Kusini waliendeleza mashambulizi yao upande wa Tanzanite na kufanikiwa 
kupata bao la tatu kupitia kwa mchezaji wake Mosili Makhoali dakika ya 
61.
Uzoefu
 wa Afrika Kusini ulionekana dhahiri kwani waliliandama lango la 
Tanzanite kila mara lakini golikipa Najiat Abbas alikuweza kupangua 
mashuti kadhaa na mengine kuishia nje lakini uzembe wa mabeki uliweza 
kusababisha kufungwa bao la nne dakika ya 78 kupitia kwa Mosil Makhoali.

Akizungumza
 baada ya mchezo kumalizika, Waziri wa habari, vijana michezo na 
Utamaduni, Fenella Mukangara aliwataka wachezaji kutolia kwani mwanamke 
jasiri anapanga nini afanye baada ya alichotangulia kukifanya hivyo kwa 
pamoja na benchi la ufundi wakae watathimini walipokosea ili wafanye 
marekebisho kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Category: tanzania
 


 
 
 
0 comments