SPURS YAZINDUKA, ADEBAYOR APIGA MAWILI WAKISHINDA 3-2 UGENINI, EVERTON YAICHINJA 2-1 SWANSEA NYUMBANI!!
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
MTU
aliyesahaulika, Emmanuel Adebayor amepiga mabao mawili katika ushindi
wa 3-2 dhidi ya Southampton na kuongeza matumaini ya kocha wa muda wa
Tottenham Hospurs Tim Sherwood kupata kazi ya kudumu.
Southampton
wakiwa nyumbani walikuwa wa kwanza kutikisha nyavu za Spurs katika
dakika ya 13 kupitia kwa Adam Lallana, lakini dakika ya 25, mshambuliaji
nyota wa Spurs raia wa Togo, Emmanuel Adebayor aliisawazishia timu yake
bao hilo.
Mpaka dakika 45 zinamalizika, ubao wa matangazo ulikuwa unasomeka 1-1.
Kipindi
cha pili Spurs walikuja juu ya katika dakika ya 54, Jos Hooiveld
alifunga bao la pili, lakini halikudumu kwani dakika tano tu
baadaye, Rickie Lambert aliisawazisha bao hilo.
Dakika ya 64, Adebayor aliwainua vitini mashabiki wa Spurs baada ya kufunga bao la tatu na la ushindi.
Spurs
waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kula kisago cha mabao 5-0
jumapili iliyopita kutoka kwa Liverpool na kusababisha kocha mkuu Andre
Villas-Boas kuoneshwa mlango wa kutokea kabla ya saa 24 kutimia tangu
ale kipongo hicho.
Sherwood,
aliyekuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya mpira wa klabu ya Tottenham
alikabidhiwa majukumu ya kuongoza kikosi hicho. Alifungwa katika kombe
la ligi `Capital One` na West Ham katikati ya wiki, na leo hii Adebayor
amempa matumaini baada ya kuongoza timu katika ushindi wa 3-2 ugenini
dimba la St Mary.
Mkali
wa kufumania nyavu: Emmanuel Adebayor aliwapunguza kasi mashabiki wa
Southampton baada ya kuisawazishia bao la kwanza Spurs
Goooooo! Adebayor akifunga bao matata baada ya kupokea pande kutoka kwa Soldado
Afadhali: Sherwood akishangilia bao lao la kwanza, lakini hataki kuwa mtu wa muda mfupi
Kama maagizo vile!: Mwamuzi, Chris Foy akimtazama Adebayor aliyekuwa akicheza mbele yake baada ya kufunga
Kikosi
cha Southampton: Gazzaniga 6, Chambers 7, Hooiveld 5, Lovren 6, Fox 5
(Gallagher 78 min); Schneiderlin 6, Davis 6 (Ramirez 69, 5), Cork 6
(Ward-Prowse 63, 6); Lallana 8, Lambert 6, Rodriguez 5.
Kikosi
cha Spurs: Lloris 6; Walker 7, Dawson 7, Chiriches 6, Rose 6; Lamela 5
(Chadli 60, 7), Eriksen 6, Dembele 5 (Bentaleb 50, 7), Sigurdsson 6;
Adebayor 8, Soldado 6 (Defoe 85).
Bao la kuongoza: Adam Lallana akishangilia baada ya kufunga bao la kuongoza kwa Southampton katika dakika ya 13
Bunduki: Lallana akipiga shuti umbali wa mita 25 na kuandika bao kimiani
Katika mchezo mwingine, Swansea City wakiwa nyumbani wamefungwa mabao 2-1 dhidi ya Everton.
Everton
walikuwa wa kwanza kuliona lango la wenyeji wao katika dakika ya 66
kupitia kwa Seamus Coleman akipokea pasi kutoka kwa James McCarthy.
Bryan
Oviedo katika dakika ya 70 aliisawazishia Swansea bao hilo, lakini
jahazi lao likazama dakika ya 84′ kupitia kwa Ross Barkley
Category: uingereza
0 comments