MESSI AUWASHA MOTO MPYAA BARCELONA
MSHAMBULIAJI Lionel Messi amewasha moto Barcelona baada ya kumuambia Mkurugenzi wake hajui lolote kuhusu soka.
Maelezo hayo ni majibu kwa Javier Faus
ambaye wiki mbili zilizopita alisema kwamba Barcelona haina sababu ya
kuketi chini na mwanasoka huyo kujadili Mkataba wake wa sasa.
Amejibu: Lionel Messi
amesema Mkurugenzi wa Barcelona, Javier Faus hajui lolote kuhusu soka
baada ya kusema hakuna haja ya kujadili Mkataba wa sasa wa Muargentina
huyo
Akizungumza na Redio ya Catalan, RAC1 kutoka
Argentina, Messi alisema: "Barcelona ni klabu bora duniani,
inawakilishwa na wajumbe bora wa bodi pia. Senor [Javier] Faus ni mtu
ambaye hajui lolote kuhusu soka na anataka kuongoza Barcelona kama
biashara, ambayo siyo,".
Alisema: "Mbali na hayo, ningemkumbusha
kwamba hata hakuna mtu yeyote kutoka kambi yangu ameulizia kuhusu
ongezeko lolote la mshahara na anafahamu hilo,".
Mwana wa dhahabu: Messi ni bidhaa adimu ndani ya Barca na ndiye mahinsi wa Kiatu cha Dhahabu Ulaya mwaka 2013
Category: uingereza
0 comments