CRISTIANO RONALDO AZUNGUMZIA UGUMU WA KUNDI WALILOPANGWA URENO KOMBE LA DUNIA
Katika
droo ya kupanga makundi ya kombe la dunia iliyofanyika Ijumaa iliyopita
ulimwengu ulishuhudia kikosi cha Paul Bento kikipangwa katika kundi
gumu la (Group G), kwa pamoja na Ujerumani, Ghana na USA - kundi pekee
lenye timu zote nne zilizopita kwenda kwenye hatua ya mtoano katika
michuano iliyopita ya kombe la dunia 2010.
Nahodha
wa Ureno, akiongea mbele ya wachezaji wake wa Madrid, Marcelo, Karim
Benzema, Luka Modric, Angel Di Maria na Iker Casillas jana jumapili
alisema kwamba hakuangalia droo hiyo moja kwa moja lakini alikuwa ana
ufahamu changamoto ngumu nchi yake ilizokuwanazo mapka kuweza kuingia
katika hatua ya 16 bora kwenye mashindano yaliyopita.
"Kiukweli,
sikuangalia moja kwa moja droo ile," Ronaldo alisema. "Nilikuwa
nimelala. Ni kundi gumu pamoja na Ujerumani, ambao ni moja ya timu
zinazopewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa, na USA pamoja na Ghana, ambazo
ni timu nzuri pia. Kufuzu kwenda hatua ya pili ni kipaumbele cha kwanza
na tutaona kitakachotokea. Tunaweza kabisa kufuzu kwenye kundi lile,
lakini kujiamini na umakini ni vitu muhimu. Inategemea na sisi kama
timu. Ninatumaini Ureno inaweza kufika mbali."
Hat
trick ya Ronaldo katika mchezo wa kugombea kufuzu dhidi ya Sweden
uliwahahkikishia Ureno nafasi ya kufuzu kwenda Brazil, lakini hakujihisi
kuwa na mzigo wowote mabegani mwake kama kiongozi wa timu uwanjani.
"Malengo
yangu siku zote yamekuwa yale yale. Kujaribu kufanya kila kitu kuisadia
nchi yangu. Binafsi mara zote nimekuwa nikijitahidi kwa ubora wangu
wote kucheza kwa juhudi, kufunga mabao na kujitoa kwa yote."
Mshambuliaji
huyo pia kasema kwamba hajamuuliza nahodha wake wa Real Madrid na timu
ya taifa ya Spain Iker Casillas inakuwaga namna gani pale unapopata
nafasi ya kubeba kombe la dunia, lakini anadhani kwamba ni jambo la aina
yake kama alivyojisikia wakati aliposhinda kombe la ubingwa wa ulaya na
Manchester United mwaka 2008.
"Sihitaji
kumuuliza. Nina akili, nafahamu umuhimu wa kubeba mataji muhimu. Kwenye
level ya klabu, nafahamu namna inavyokuwa kubeba ubingwa wa Champions
League na ninaamini kubeba ubingwa wa kombe la dunia ni jambo zuri
zaidi. Ndoto ambayo wachezaji wenzangu na mimi tunayo ni kubeba ubingwa
wa kombe la ulaya na dunia kwa kwa ajili ya nchi yetu, lakini inabidi
tuweke miguu chini na kujituma kutimiza ndoto zetu. Ni timu bora pekee
zinazoweza kushinda na ninaamini kwamba Ureno inaweza kuwa moja ya timu
bora."
Category: uingereza
0 comments