YANGA YAKALIA USUKANI WA LIGI KUU BARA KWA KUFIKISHA POINTI 25, YAWALAMBA JKT RUVU 4-0 TAIFA, NGASSA BALAA!!

Unknown | 9:03 PM | 0 comments

 


 Mshambuliaji wa Yanga, aliyeingia kuchukua nafasi ya Didier Kavumbagu, Jerry Tegete, akimtoka beki wa JKT Ruvu, Nashon Naftal, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeshinda mabao 4-0, mabao mawili yakifungwa na Mrisho Ngasa, katika dakika za 4 na 23 kipindi cha kwanza, bao la tatu limefungwa na Oscra Joshuo, katika dakika ya 50 na bao la nne limefungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 86.
 Jerry Tegete (kushoto) akishangilia bao lake kwa staili ya kunong'oneza, huku akipongezwa na Simon Msuva (kulia) na Mrisho Ngasa.
 Didier Kavumbagu, akimfinya beki wa JKT Ruvu Mussa Zubery, wakati wa mtanange huo.
 Simon Msuva (kulia) akiruka daruga la beki wa JKT Ruvu na kuambaa na mpira, ambapo alifanikiwa kutoa pasi nzuri iliyomkuta Hamis Kiiza, aliyeshindwa kupata bao la wazi.
 Sehemu ya Jukwaa la mashabiki wa Simba, likiwa tupu, haikuweza kufahamika sababu za kutohudhuria kama ilivyokuwa katika mechi za siku za nyuma.
 Mashabiki wa Yanga, ilikuwa ni shangwe......
 Hamis Kiiza, akipiga mpira wa kichwa na kusababisha heka heka langoni mwa JKT Ruvu.
Mrisho Ngasa, akiwafinya mabeki wa JKT Ruvu.....

 Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa, akiruka kupiga mpira wa kichwa na kufunga bao la pili katika dakika ya 13, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Mabao mawili yamefungwa na Ngasa ambapo goli la kwanza akifunga katika dakika ya 4 kwa suti kali alilopiga akiwa nje ya 18 baada ya pasi nzuri ya Didier Kavumbagu. Bao la tatu limefungwa na beki wa kushoto wa yanga, Oscar Joshua, katika dakika ya 50.
 Kipa wa JKT Ruvu, akishangaa na kulalamika na mabeki wake baada ya kufungwa bao la pili.
Mrisho Ngasa, akishangilia bao lake la pili, akipewa kampani na beki wake Canavaro.
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaama wamebarizi kieleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara kufuatia ushindi wa mabao 4-0 kwenye uwanja wa Taifa jioni hii dhidi ya timu iliyoanza ligi kwa kishindo, lakini kwa sasa mambo ni mdobwedo kwao, JKT Ruvu ya mkoani Pwani.
Ushindi huo muhimu inaifanya Yanga kufikikisha pointi 25, tofauti na timu mbili za Azam fc na Mbeya City zenye pointi 23 kila moja, lakini yawezekana Yanga wakaa kileleni kwa saa tu endapo timu hizo zitashinda katika michezo yao ya wikiendi hii.
Mabao ya Yanga leo hii yamefungwa na winga hatari wa klabu hiyo, Mrisho Khalfan Ngassa aliyefunga mawili ambapo katika dakika ya tatu alipiga shuti kali baada ya kufanikiwa kuwachomoka walinzi wa JKT Ruvu  na dakika ya 12 aliunganisha kama kawaida mpira wa kurusha wa beki Mbuyu Twite na kuleta shangwe kubwa kwa mashabiki waliofurika uwanjani.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zikimalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-0, lakini kiukweli JKT Ruvu ndio walicheza soka zuri na la uhakika, ila Yanga waliwazidi kwa hesabu nzuri za mashambulizi ya haraka.
DSC_0026Kipindi cha pili kilipoanza, Yanga waliendelea kulisakama lango la JKT Ruvu na Beki Oscar Samwel Joshua aliandika bao la tatu  dakika ya pili ya kipindi cha pili akiunganisha kona  murua iliyochongwa na winga mwenye kasi kubwa,  Simon Msuva.
Kikosi cha Yanga SC:  Deo Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite/Ibrahim Job dk45, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Relianst Lusajo dk78, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete dk64, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza.
Kikosi cha JKT Ruvu; Sadick Mecks, Mussa Zuberi, Kessy Mapande, Omar Mtaki, Damas Makwaya/Richard Msenyi dk64, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Haruna Adolph, Paul Ndauka, Samuel Kamutu/Abdallah Bunu dk 64 na Sosthenes Manyasi/Emmanuel Pius dk59.  
Msuva

Raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo ipo katika raundi yake ya 12 inaendelea kesho (Novemba 2 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji minne tofauti.
Mgambo Shooting na Coastal Union zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Mbeya City na Ashanti United zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Oljoro kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons.
 
Credit: Full shangwe na Mafoto blog

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments