TASWA YAPONGEZA UONGOZI MPYA WA TFF CHINI YA JAMAL MALINZI

Tunaungana
na wapenda michezo na Watanzania kwa ujumla kuitakia kila la heri
Kamati ya Utendaji ya TFF na shirikisho hilo kwa ujumla chini ya Rais
mpya Jamal Malinzi na Makamu wake, Wallace Karia.
TASWA
inaamini Malinzi, Karia na wajumbe wao ni wazoefu na ni watu wenye
kujua mambo mengi yanayohusu mpira wa miguu nchini, hivyo tunaamini
watakuwa viongozi wazuri kwa nafasi zao katika kuhakikisha shirikisho
hilo linasonga mbele.
Tunawatakia
kila la heri Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji, huku tukiamini
hawatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF waliowaamini kushika
nafasi hizo.
TASWA
na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla hapa nchini tunaahidi
kuwapa ushirikiano wa kutosha ili watekeleze majukumu yao ipasavyo.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
30/10/2013
Category: tanzania
0 comments