PICHA ZA MECHI ZA LEO ZA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA,CHELSEA YAPIGA "FOUR OCLOCK"

Unknown | 7:32 AM | 0 comments


ARSENAL WAKISHANGILIA BAO LA OZIL..

MATA AKIPAMBANA..
Chelsea imeamka katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibandua Steau Bucharesti kwa mabao 4-0 ambayo ilikuwa nyumbani.
Chelsea  imeibuka na ushindi huo baada ya mechi yake ya mwisho ya kundi E kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Basle wakiwa jijini London.
RAMIRES AKIFUNGA BAO LA KWANZA
Mabo ya Chelsea, yote mawili yalifungwa na Ramires huku moja beki Geogievski akijifunga na mkongwe Lampard akahitimisha ‘four oclock’.

Upande mwingine, Arsenal wakiwa nyumbani walionyesha kuwa kweli msimu huu ‘wamesimama’ baada ya kuichosha Napoli ya Italia kwa kipigo cha mabao 2-0.

Mesut Ozil alianza kuonyesha cheche zake katika dakika ya 8 tu na Olvier Giroud akapachika la pili katika dakika ya 15.


Haikuwa mechi lahisi kwa kuwa wageni hao walionyesha wabishi licha ya kumkosa Gonzalo Higuain ambaye ni majeruhi.

Barcelona ikiwa ugenini bila ya Lionel Messi ikahaha na kupata ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Celtic, mfungaji akiwa ni Cesc Fabregas.
MATOKEO MENGINE:
Basel 0 Schalke 1
Borussia Dortmund 3 Marseile 0
Zenit Petersburg 0 Austria Wien 0
FC Porto 1 Atletico Madrid 2

Ajax 1 Ac Milan 1

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments