"MIKOKO" YA HATARI INAYOMILIKIWA NA ETO'O
MSHAMBULIAJI Samuel Eto'o ambaye
Watanzania wanamuita shemeji baada ya kukutwa na skendo ya kutembea na
binti mmoja wa Dar es Salaam alipokuja na timu yake ya taifa miaka
mitano iyopita, ametumia mshahara wake kununua magari ya kifahari yenye
thamani ya jumla ya Pauni Milioni 4.
Gari mpya ya mshambuliaji huyo wa
Chelsea ina thamani ya Pauni Milioni 1.55 ambayo ni aina ya Bugatti
Veyron ambayo alihamia nayo London pamoja na nyingine tatu akitokea
Anzhi msimu huu.
Pamoja na Veyron, Eto'o ametumia Pauni Milioni 1.25 kununua Aston Martin One-77, kwa mujibu wa gazeti la The Sun.
Mshambuliaji huyo wa Cameroon mwenye umri wa miaka 31, pia amenunua
gari la maraha aina ya Maybach Xenatec kwa Pauni 750,000 na Aston Martin
V12 Zagato kwa Pauni 450,000.

Kazini: Samuel Eto'o alitokea benchi na kuisaidia Chelsea kushinda 4-0 dhidi ya Steaua Bucharest

Kitu cha hatari: Eto'o anamiliki Bugatti Veyron kama hii pichani

Si mbaya: Mcameroon huyo pia anamiliki gari la Pauni Milioni 1.25 aina yaAston Martin One-77
Eto'o wakati wote amekuwa mpenzi wa
magari na imewahi kuripotiwa alimpa zawadi ya gari mshambuliaji wa
zamani wa Cameroon, Roger Milla wakati wa Krisimasi mwaka 2010.
Alisema: "Napenda kuwa na gari chache kwa sababu inanipa nafasi ya kuchagua na haimuumizi yeyote.
"Kuwa mwenye furaha, kitu cha kwanza ni kufurahi na nafsi yako, na nina furaha,".

Kazi nzuri: Eto'o pia anamiliki Maybach Xenatec Coupe yenye thamani ya Pauni 750,000

Na nyingine... Magari ya Eto'o yenye
thamani ya jumla ya Pauni Milioni 4 ni pamoja na Aston Martin V12
Zagato, yenye thamani ya Pauni 450,000
Category: uingereza
0 comments