MECHI ZA YANGA, SIMBA ZAINGIZA MIL 182/-
Mechi za Yanga na Simba za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zilizochezwa wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam zimeingiza jumla ya sh. 182,103,000.
Yanga
katika mechi yake dhidi ya Ruvu Shooting iliyochezwa Jumamosi (Septemba
28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa
bao 1-0 imeingiza sh. 94,202,000.
Watazamaji
16,492 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo kila klabu
ilipata mgawo wa sh. 22,630,921.58. Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000, na Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,369,796.61.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,507,248.26,
tiketi sh. 3,117,215, gharama za mechi sh. 6,904,348.96, Kamati ya Ligi
sh. 6,904,348.96, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
3,452,174.48 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,685,024.59.
Nayo
Simba ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu katika
mechi iliyochezwa Jumapili (Septemba 29 mwaka huu) katika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 87,901,000.
Watazamaji
waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 41 walikuwa
15,780. Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 21,051,025.92
wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
13,408,627.12.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 10,703,911.48,
tiketi sh. 3,132,963, gharama za mechi sh. 6,422,346.89, Kamati ya Ligi
sh. 6,422,346.89, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
3,211,173.44, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,248,789.67 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh.
1,248,789.67.
Wakati
huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya Mbeya City na Coastal
Union iliyochezwa Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 16,959,000 huku kila klabu
ikipata sh. 4,035,229.
Category: tanzania
0 comments