Home �
tanzania
� MALINZI AMBWAGA NYAMLANI URAIS TFF
Unknown |
7:12 AM |
0
comments
Na
Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
JAMAL Emil
Malinzi, usiku huu ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya
kupata kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne
Nyamlani.Katika uchaguzi huo
uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia
alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa kupata kura 67 akiwashinda
Nassib Ramadhani kura 52 na Imani Madega sita.
|
Huyu ndiye Rais wenu mpya TFF; Rais
aliyemaliza muda wake TFF, Leodegar Tenga kushoto akimtambulisha Jamal Malinzi
kuliakuwa Rais mpya wa shirikisho hilo usiku nwa kuamkia leo ukumbi wa NSSF
Water Front, Dar es Salaam |
Katika
nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa zamani wa Simba SC Wilfred Kidau
amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, Omar Abdulkadir kura 10 na
Alex Kabuzelia kura nne.
Kanda 12;
Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura
54.
Kanda ya 11
Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala kura tano,
Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya
10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata nne na
Stewart Nasima 58.Kanda ya tisa Othman Kambi
aliyepata kura 84 yeye amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati James
|
Tenga akimkabidhi mpira Malinzi
kuashiria yeye ndiye kiongozi mpya mkuu wa soka
nchini |
|
Anampa shada la maua ishara ya
kumuachia madaraka |
|
Kwaherini; Tenga akiwaaga
Wajumbe |
Mhagama
aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda aliyepata kura 11 na Kanda ya nane,
Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52.Kanda ya Tano, Ahmed Iddi
Mgoyi aliyepata kura 92 amemshinda Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34, wakati
Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa.
|
Anamkabidhi Katiba ya
TFF |
|
Anapongezwa na Mwenyekiti wa Azam
FC, Sheikh Said Muhammad Said
Abeid |
Eley Mbise
amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai. Mbasha
Matutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61, wakati
Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati kura 11,
Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 na Kanda namba moja, Karilo
Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.
|
Kamati mpya ya Utendaji
TFF |
|
Wadau Musley Ruwey kushoto na Said
Tuliy kulia walikuwepo hadi mwisho |
Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Category:
tanzania
0 comments