SIMBA YATOKA SARE YA 2-2 NYUMBANI NA WATOTO WA MBEYA CITY
Timu
ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo imecheshwa kwata na Vijana wa
Mbeya city na kuvtwa shati katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
uliochezwa kwenye Uwanja wa taifa.
Katika
mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2, ambapo mchezaji wa
Simba, Amis Tambwe mbaye wiki hii alinukuliwa na baadhi ya magazeti
akijinadi kuwa mfungaji bora wa msimu huu, ameweza kuifungia timu yake
mabao yote mawili katika dakika za 29 na 33.
Nao
Mbeya City, timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya inayofundishwa na Juma
Mwambusi, bao la kipindi cha kwanza lilifungwa na Paul Nonga dakika ya
37, wakati la kusawazisha lilifungwa na Richard Peter dakika ya 69.
Category: tanzania
0 comments