Home �
tanzania
� Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo azindua Rocky City Marathon
Unknown |
10:21 PM |
0
comments
 |
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa awamu ya tano ya Mbio za Rock City Marathon
2013, leo Jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Capital
Plus International (CPI), Dkt. Hellen Otaru Okoedion. Mbio hizo zinazoandaliwa
na kuratibiwa na CIP zinatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza tarehe 27 Oktoba, mwaka huu.
|
 |
Katibu Mkuu wa Chama
cha Wanariadha Tanzania, Bw. Suleiman Nyambui (katikati) akimueleza jambo Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante
Ole Gabriel baada ya uzinduzi wa awamu ya tano ya mbio za Rock City Marathon
leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Precision
Air, Bibi Linda Chiza ambao ni mmoja wa wadhamini wa mbio hizo.
|
 |
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati
aliyevaa suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji, wadhamini na
watendaji wa Baraza la Michezo Tanzania wakati wa uzinduzi wa awamu ya tano ya
mbio za Rock City Marathon leo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bw. Dioniz Malinzi, wa pili ni Kaimu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Capital Plus International, Dkt. Hellen Otaru Okoedion
na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa BMT, Bw. Henry Lihaya. Mbio hizo zinazoandaliwa
na kampuni ya Capital Plus International zinatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza
tarehe 27 Oktoba, mwaka huu.
(Picha zote na Concilia Niyibitanga
|
Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Category:
tanzania
0 comments