LIVERPOOL YAPATA POINTI MOJA KWA SWANSEA
Liverpool
imetoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea katika mechi ya Ligi Kuu England
iliyomalizika hivi punde.
Sare hiyo imeifanya Liverpool ipae hadi kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 10, Arsenal wanafuatia wakiwa na pointi 9.
Sare hiyo imeifanya Liverpool ipae hadi kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 10, Arsenal wanafuatia wakiwa na pointi 9.
Mechi
hiyo ilikuwa tamu na ya kuvutia kutokana na mchezo kuwa wa kuvutia na ufundi
mwingi kutoka kila upande.
Wenyeji
Swansea ndiyo waliuanza mchezo kwa kasi na kupata bao katika dakika ya 2
mfungaji akiwa kiungo wa zamani wa Liverpool, Jonjo
Shelvey.
Lakini
Liverpool walisawazisha dakika mbili baadaye kupitia Danny Sturridge aliyejiunga
na timu hiyo akitokea Chelsea.
Baada
ya bao hilo, Liverpool waliendelea kuwa ‘tatizo’ kwa Swansea wakishambulia zaidi
kwa mipira mirefu, hata hivyo mabeki wa timu hiyo walikuwa makini
kuokoa.
Victor
Moses aliifungia Liverpool bao la pili katika dakika ya 87 ambalo lilifanya
matokeo yawe 2-1 hadi mapumziko.
Mwanzo
wa kipindi cha pili, mambo yalibadilika na Swansea ndiyo walionekana kuutawala
mchezo na kuipa Liverpool wakati mgumu hadi Michu alipofunga bao la kusawazisha
katika dakika ya 63 baada ya kupokea pasi nzuri ya kichwa kutoka kwa
Shelvey.
Baada
ya hapo, Liverpool waliendelea kuwa katika wakati mgumu kutokana na mashambulizi
mfululizo ya Swansea waliokuwa wamepania kupata ushindi wa kwanza msimu
huu.
Category: uingereza
0 comments