CRISTIANO RONALDO ASAINI MKATABA MPYA NDIYE MWANASOKA ANAYELIPWA ZAIDI DUNIANI KWA SASA
MRENO Cristiano Ronaldo amesaini Mkataba
mnono wa miaka mitano kuendelea kuichezea Real Madrid, wenye thamani ya
Pauni Milioni 76 (zaidi ya Euro Milioni 90) inayomfanya awe
Ronaldo amesaini Mkataba huo Santiago
Bernabeu leo na rais wa klabu, Florentino Perez siku moja baada ya
kufunga Madrid ikitoa sare ya 2-2 na Villarreal.
Kiwango hicho kinamfanya awe analipwa
karibu mara mbili ya malipo ya Gareth Bale na kinarejesha heshima yake
baada ya kupoteza hadhi ya mwanasoka ghali duniani, kufuatia Real
kumnunua Bale kwa Pauni Milioni 86.
Dole tupu: Cristiano Ronaldo akiwa na Rais Florentino Perez baada ya sherehe za kuutangaza Mkataba wake mpya Santiago Bernabeu

Haendi popote: Ronaldo akiwa Santiago Bernabeu kusaini Mkataba mpya

Mambo yamekuwa: Ronaldo akiwa na Rais Florentino Perez baada ya kusaini Mkataba mpya
Katika mkataba huo mpya, Real itamlipa
Ronaldo Pauni Milioni 15 kwa mwaka baada ya makato ya kodi na nje ya
posho mbalimbali. Bale analipwa Pauni Milioni 8.3 kwa msimu na mshahara
mpya wa Ronaldo unamfanya azidi kwa Pauni 850,000 kwa mwaka,
mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic.
Pia inazima kabisa ndoto za klabu yake ya zamani Manchester United kumrejesha Ronaldo Old Trafford.
"Nina furaha haswa hapa,"alisema. "Nitakuwa hapa kwa miaka mitano zaidi. Nataka kushinda mataji katika klabu hii.


Mkataba mpya: Cristiano Ronaldo amesaini Mkataba mpya mnono Real Madrid

Mkataba wa Real: Ronaldo amesema anataka kumalizia soka yake Madrid

Wote wanatabasamu: Ronaldo akizungumza na vyombo vya Habari Hispania baada ya kusaini Mkataba mpya
"Nawakubali
mashabiki wanavyonipenda hapa. Nina furaha, nataka kuonyesha mavitu
yangu uwanjani. Nitakuwa mkweli kwako- kila mmoja anajua nilikuwa
Manchester kwa miaka sita. Manchester ni ya kale sasa. Sasa klabu yangu
ni Real Madrid. Hii ni nyumbani, familia yangu iko hapa na nina furaha
haswa hapa.
"Naziheshimu klabu zote zilizonitaka.
Lakini wakati wote wanafahamu uamuzi wangu, kwamba lengo langu ni kuwa
hapa na kucheza labda, pengine, mwisho wa maisha ya soka. "Yajayo hakuna ajuaye,".
Category: uingereza
0 comments