Yanga yawagonga Waarabu 1 - 0 Kombe la Shirikisho
Mabingwa wa Ligi kuu ya Soka Tanzania bara Yanga wameibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Wawakilishi wa Algeria MC Alger katika mchezo wa hatua ya mtoano katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Iliwachukua dakika 9 tu Yanga kufanya shambulizi la nguvu langoni mwa MC Alger huku Obrey Chirwa akikosa bao la wazi baada ya shuti lake kudakwa na kipa wa Mc Alger lakini pia dakika ya 27 na 42 pia Chirwa alishindwa kuwapa Yanga goli la kuongoza.
Kwa upande wa wageni MC Alger walifanya
Mashambulizi yao kupitia kwa Goveri Kaled ambaye alikosa nafasi ya wazi kwa kupiga shuti na mpira kutoka nje ikiwa pasi nzuri ya derarya Warid.
Bao pekee la Yanga katika mchezo wa leo lilifungwa na kiungo Thaban Kamusoko dakika ya 60 akipiga shuti kali baada ya kazi nzuri ya Haruna Niyonzima .
Kwa matokeo hayo sasa Yanga itabidi wapate sare tu katika mechi ya marudiano wiki ijayo ili kuweza kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ya kombe la shirikisho ambayo ni ya pili kwa ukubwa katika ngazi ya klabu barani Afrika.
Category: tanzania
0 comments