Yanga yabanwa mbavu na Mtibwa
Mabingwa wa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara Yanga wameshindwa kukalia kiti cha uongozi wa ligi kuu Tanzania bara inayoendelea baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Jamhuri mjini Morogoro ulikua ni mchezo muhimu kwa mabingwa hao watetezi kushinda ili kuweza kukalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo baada ya Simba nao kutoka sare ya bao 2-2 jana na Mbeya City.
Yanga itabidi wajilaumu wenyewe kwani walipata nafasi nne za kufunga ikiwa ni pamoja na penati lakini Simon Msuva akapaisha juu.
Kwa matokeo hayo sasa Simba inaendelea kuongoza ligi hiyo ikifikisha pointi 55 huku Yanga ikishika nafasi ya pili kwa pointi 53.
Category: tanzania
0 comments