Mbwana Samattah apiga 2 Genk

Unknown | 11:12 AM | 0 comments

Star wa soka Tanzania na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta, amefunga magoli mawili usiku wa March 4, 2017 kwenye mechi ya ligi kuu ya Ubelgiji wakati timu yake ya KRC Genk ikicheza nyumbani dhidi ya Club Brugge ambao ndio vinara wa ligi.

Samatta alipasia nyavu dakika ya 5 na 42 kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri zilizofanywa na Malinovsky pamoja na Alejandro Pozuelo huku goli pekee la wapinzani wao likifungwa na  Izquierdo dakika ya 43.

Magoli ya Samatta yaliisaidia Genk kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 na kufikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 29 na kubakia kwenye nafasi ya nane ya msimamo wa ligi yenye timu 1

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments