Man United yadroo 1-1
Katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford timu hizo zikitoka sare ya kufungana bao 1-1. Man United walitangulia kwa bao la Marcos Rojo dakika ya 23 kabla ya Joshua King kuisawazishia Bournemouth dakika ya 40 kwa penalti kabla ya kipa Artur Boruc kuicheza penalti ya Zlatan Ibrahimovic dakika ya 72 kuwanyima Mashetani Wekundu ushindi wa nyumbani. Bournemouth ilimaliza pungufu baada ya Andrew Surman kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45
Category: uingereza
0 comments