Home �
uingereza
� Lampard astaafu rasmi soka
Unknown |
9:04 PM |
0
comments
KIUNGO Frank Lampard ametangaza kustaafu soka ya ushindnai baada ya zaidi ya miongo miwili ya kuwa kazini.Gwiji huyo wa Chelsea, ambaye alishinda heshima zote kubwa wakati wake akiwa kazini Stamford Bridge, ameamua kustaafu baada ya kuondoka New York City ya Ligi Kuu ya Marekani mwishoni mwa msimu.Lampard, mwenye umri wa miaka 38 sasa, ametangaza kustaafu kwake kupitia ukurasa wake wak Instagram ambako ameposti ujumbe wa kuwashukuru wote waliochangua mafanikio yake ikiwemo kuichezea mechi 106 timu yake ya taifa ya England.
HISTORIA YA LAMPARD
1995-2001: West Ham - mechi 187/mabao 39
1995-96: Swansea (mkopo) - mechi 11/bao 1
2001-2014: Chelsea - mechi 649/mabao 211
2014-15: Man City - mechi 38/mabao 8
2015-16: New York City - mechi 19/mabao 12
1999-2014: England - mechi 106/mabao 29
JUMLA: mechi 1010/mabao 300
MATAJI ALIYOTWAA LAMPARD
Chelsea
Ligi Kuu x3: 2004-05, 2005-06, 2009-10
Kombe la FA x4: 2006-07, 2008-09, 2009-10, 2012
Kombe la Ligi x2: 2004-05, 2006-07
Ngao ya Jamii
x2: 2005, 2009
Ligi ya Mabingwa: 2011-12
Europa League: 2012-13
West Ham
Intertoto Cup: 1999
Lampard ameishukuru familia yake, akiwemo mkewe Christine ambaye ameandika ujumbe wa kujivunia mumewe kwenye ukurasa wake wa Instagram pamoja na picha ya 'bwana mkubwa huyo'.
Lampard amezishukuru pia klabu alizochezea enzi zake kuanzia West Ham katikati ya miaka tisini. Amesema Chelsea, ambako ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, mannde ya FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya zaidi ya miaka 13 daima itabakia kuwa na nafasi kubwa moyoni mwake na pia akazishukuru Manchester City na New York City.
Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Category:
uingereza
0 comments