Simba yatawala Ligi Kuu Tanzania Bara

Unknown | 8:56 PM | 0 comments

Mzunguko wa 8 wa ligi kuu Tanzania bara unaendelea Jumatano na Alhamisi wiki hii kwa michezo kadhaa kuchezwa katika viwanja mbalimbali Tanzania bara.


Wekundu wa Msimbazi Simba ambao watacheza na Mbeya City Jumatano ndiyo wanaoongoza ligi hiyo huku Majimaji licha ya kupata ushindi wake wa kwanza juzi dhidi ya Mbao FC ya Mwanza bado wanakamata mkia wa ligi hiyo.

www.wapendasoka.com imeangaza mambo kadhaa kuhusu ligi hiyo kitakwimu na haya ni baadhi tu ya yale tuliyokuandalia

● Timu 3 za Juu katika msimamo wa ligi.
1. Simba S.C - Pointi 17
2. Stand United - Pointi 16
3. Mtibwa Sugar - Pointi 14

● Timu iliyoshinda Mechi nyingi.
1. Simba S.C - Mechi 5
2. Stand United - Mechi 4
3. Mtibwa Sugar - Mechi 4

● Timu iliyofungwa Mechi chache.
1. Simba S.C - Mechi 0
2. Stand United - Mechi 0
3. Tanzania Prisons na Yanga SC  - Mechi 1

● Timu iliyofunga magoli mengi.
1. Simba S.C - Magoli 13
2. Azam FC - Magoli 10
3. Yanga S.C - Magoli 9

● Timu iliyofungwa magoli machache
1. Yanga SC - Magoli 2
2. Simba SC - Magoli 3
3. Stand United/JKT Ruvu - Magoli 3

● Wachezaji wanaaongoza kwa Ufungaji.
1. Shiza Kichuya (Simba SC) - Magoli 5
2. Amis Tambwe (Yanga SC) - Magoli 4
3. Laudit Mavugo (Simba SC) - Magoli 3

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments