Huu hapa ukweli juu ya kocha Pluijm kutimuliwa Yanga
Klabu ya Yanga inapenda kuwatangazia wanachama wote wa Young Africans Sports Club (YANGA) kuwa habari zilizoenea kwenye mitandao na magazeti juu ya mabadiliko ya benchi la ufundi wa klabu kuwa ni uzushi na sio za kweli.
Uongozi bado unamtambua Mwalimu Hans Van De Plujim kama kocha mkuu na Juma Mwambusi kama kocha msaidizi.
Uongozi unawaomba wanachama kupuuzia hizo habari popote pale wanapokutana nazo.
'YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO'
Imetolewa na Uongozi - Young Africans Sports Club
10-10-2016
Category: tanzania
0 comments