Simba yairarua Mwadui
Vinara wa ligi kuu ya Soka Tanzania bara Simba imeendelea kutoa dozi kwa kila timu inayokutana nayo baada ya kuilaza Mwadui kwa bao 3-0.
Pambano hilo lililopigwa katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga lilikua la kwanza kwa Simba katika kanda ya Ziwa lingine likipigwa katikati ya wiki ijayo dhidi ya Stand United.
Simba ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Mohamed Ibrahim kabla ya Ramadhani Kichuya hajafunga bao la pili akimalizia kazi nzuri ya Mohamed Ibrahim na mpaka mapumziko tayari Simba walikua mbele kwa bao 2-0.
Kazi iliyobaki kwa Simba kipindi cha pili ni kumalizia ushindi wao kwa kufunga bao la 3 lililofungwa na Mohamed Ibrahim na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi huo mnono kwa Simba.
Kwa matokeo hayo Simba inafikisha pointi 32 katika nafasi ya kwanza ikifatiwa na Yanga yenye pointi 24.
Category: tanzania
0 comments