Ratiba robo fainali kombe la ligi ya Uingereza yatoka ... Hii hapa ...

Unknown | 10:34 AM | 0 comments

Droo ya mechi za robo fainali ya kombe la ligi nchini England imepangwa baada tu ya kumalizika kwa pambano baina ya Man United na Man City.


Ratiba hiyo inaonyesha katika hatua ya Robo fainali Manchester United itakua tena katika dimba la Old Trafford na safari hii kucheza dhidi ya West Ham United ambayo jana iliitoa Chelsea kwa kuifunga bao 2-1.

Arsenal ambao waliitupa nje Reading wamepangwa kukutana na Southampton mechi itakayopigwa katika dimba la Emirates.

Hull City wao watakua na kazi pevu kumenyana na Newcastle United ambayo imetinga hatua hii kwa ushindi mnono wa bao 6-0.

Liverpool wenyewe baada ya kuwaondosha Tottenham Hottspur wataikaribisha Leeds United katika uwanja wa Anfield.

Mechi hizo zitachezwa tarehe 29 na 30 Novemba mwaka huu.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments