YANGA YAKOMALIWA NA NDANDA .... AZAM WATAKATA
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga wamebanwa mbavu na wenyeji Ndanda FC ya Mtwara na kulazimishwa sare tasa katika pambano la ligi kuu Tanzania bara.
Wachezaji Azam wakipasha kabla ya mchezo wao dhidi ya Prisons |
Huko Jijini Mbeya wenyeji Tanzania Prisons walikubali kukalishwa chini na Azam FC wakitandikwa bao 1-0
Bao pekee katika pambano hilo lilipatikana kipindi cha pili likifungwa na mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo Kipre Balou kwa shuti kali lililogonga mwamba wa juu wa goli na kujaa kimiani.
Category: tanzania
0 comments