Messi atakosa mechi 3 muhimu na timu yake ya Barcelona

Unknown | 10:10 AM | 0 comments

Mchezaji bora wa dunia na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi atakia nje kwa wiki 3 baada ya kupata maumivu ya nyonga jana.

Barcelona ikiwa nyumbani ilikubali kugawana pointi na Atletico Madrid mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Ivan Rakitic wa Barcelona akitangulia kufunga kabla ya Atletico kusawazisha kupitia kwa Angel Correa.

Katika mechi hiyo Barcelona walimpoteza mshambuliaji wake Huyo Lionel Messi baada ya kutoka uwanjani wakati wakiongoza kwa bao 1-0.

Kwahiyo Messi atakosa mechi 3 za Barcelona dhidi Borussia Monchenglebach Jumatano Ijayo kisha mechi mbili za La Liga dhidi ya Sporting Gijon na Celta Vigo huku akitazamiwa kurejea dimbani dhidi ya Manchester City Oktoba 19

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments